Bibi Peng Liyuan na wake wa viongozi wa nchi za Asia ya Kati watembelea ukumbi wa kihistoria
2023-05-19 22:10:13| cri
Mke wa Rais wa China Bibi Peng Li Yuan, leo asubuhi aliwaalika mke wa Rais wa Kyrgyzstan Bibi Aigul Japarova, na mke wa Rais wa Uzbekistan Bibi Ziroatkhon Mirziyoyeva, kutembelea ukumbi wa kihistoria wa Yisushe huko Xi'an, China.
Bibi Peng kwanza aliwapeleka wageni wake kwenye makumbusho ya sanaa ya opera ya Qinqiang katika ukumbi wa maonyesho ya kiutamaduni wa Yisushe, ambapo walijionea vitu vya kupendeza vinavyohusiana na opera, na pia kujionea wanamuziki wakifanya onyesho wa jadi.
Bibi Peng na wageni wake pia walijaribu kutengeneza sanaa ya vivuli kwenye ukumbi wa maonyesho na kuzungumza na wasanii wakongwe
Bibi Peng amewambia wageni wake kuwa China iko tayari kuimarisha mabadilishano ya utamaduni na ushirikiano na nchi za Asia ya Kati, na kukuza uelewa wa pamoja na urafiki kati ya watu, Peng alisema.
Bibi Japarova na Bibi Mirziyoyeva wamesema wamehisi Barabara ya Hariri imeunganisha tamaduni za Asia ya Kati na China, na kutarajia kuwa pande zote mbili zitaimarisha mabadilishano ya watu na kufundishana.