Watu 18 wauawa katika shambulizi la majambazi kusini magharibi mwa Chad
2023-05-19 08:41:07| cri

Ofisa wa eneo la Logone Mashariki, kusini-magharibi mwa Chad amesema shambulizi lililofanywa na majambazi asubuhi ya tarehe 17, limesababisha vifo vya takriban raia 12 na majambazi 6.

Vyombo vya habari vya ndani vinaamini kuwa kutokana na kuwa eneo la mashariki la Logone linapakana na Cameroon na Jamhuri ya Afrika ya Kati, kuna uwezekano kuwa washambuliaji ni wageni.