Rais wa China akutana na viongozi wa nchi za Asia ya Kati
2023-05-19 08:53:27| CRI

Rais wa China Xi Jinping jana mjini Xi’an kwa nyakati tofauti alikutana na viongozi wa nchi za Asia ya Kati wanaoshiriki kwenye Mkutano wa viongozi kati ya China na Asia ya Kati na kufanya ziara nchini China.

Alipokutana na mwenzake wa Turkmenistan Serdar Berdymukhamedov, rais Xi amesema China inapenda kushirikiana na Turkmenistan kuhimiza uhusiano kati ya nchi hizo mbili kupata maendeleo mapya, ili kuwanufaisha zaidi watu wa nchi hizo mbili.

Kwenye mazungumzo kati yake na mwenzake wa Tajikistan Emomali Rahmon, rais Xi amesema China inapenda kushirikiana na Tajikistan kuinua kwa pande zote kiwango cha ushirikiano katika sekta mbalimbali, ili kuhimiza ujenzi wa jumuiya yenye mustakabali wa pamoja kati ya pande hizo mbili ambayo ina urafiki wa kudumu, mshikamano na kunufaishana na kupata mafanikio kwa pamoja.

Kwenye mazungumzo na mwenzake wa Kyrgyz Sadyr Japarov, rais Xi amesema China inapenda kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja ya ujirani na urafiki mwema na kunufaika kwa pamoja na ustawi, ili kuchangia ustawi wa maendeleo ya nchi hizo mbili.

Alipokutana na mwenzake wa Uzbekistan Shavkat Mirziyoyev, rais Xi amesema China inapenda kushirikiana na Uzbekistan kukuza ushirikiano kwa pande zote, ili kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja kati ya pande hizo mbili.