Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania amesema Tanzania inapanga kurusha satelaiti yake na kujiunga na majirani zake Kenya na Uganda, ambao wameweza kurusha satelaiti zao katika miezi sita iliyopita.
Rais Hassan amesema mazungumzo ya kurusha satelaiti yameanza.
Kenya ilirusha satelaiti yake ya kwanza mwezi Aprili kwa kushirikiana na kampuni ya SpaceX. Satelaiti hii inaweza kukusanya data za kilimo na mazingira, pamoja na mafuriko, ukame na moto wa msituni.
Uganda ilirusha satelaiti yake ya kwanza mwaka jana kwenye Kituo cha anga ya juu cha kimataifa.