Idadi ya kesi zinazoshukiwa kuwa za kipindupindu nchini Zimbabwe imezidi 1,000, na 288 kati ya hizo zimethibitishwa kuwa na ugonjwa huo, huku watu 6 wakifariki katika mlipuko wa hivi karibuni wa ugonjwa huo.
Wizara ya Afya na Huduma ya Watoto nchini humo imesema, watu 51 wamelazwa hospitali kutokana na ugonjwa huo mpaka kufikia jumatatu wiki hii, na kuongeza kuwa mji mkuu wa Zimbabwe, Harare, ni moja ya miji iliyoathiriwa zaidi na ugonjwa huo.
Takwimu zilizotolewa na serikali ya nchi hiyo zinaonyesha kuwa, mkoa wa Matabeleland Kusini una kesi 91 zilizothibitishwa kuwa na kipindupindu, ukifuatiwa na mkoa wa Manicalanda wenye kesi 89, na Harare kesi 80.