Afrika inatafuta nafasi mpya huku nchi tajiri zikiangalia raslimali zake
2023-05-22 21:38:56| cri

Kamishna wa Umoja wa Afrika anayeshughulikia mambo ya Biashara Bw. Robert Muchanga, amesema Afrika haitakubali kuendelea tu kuwa chanzo cha malighafi kwa dunia nzima, na badala yake inataka mustakabali wa "mahusiano ya kweli na yenye manufaa kwa pande zote" na washirika wake wa kibiashara.

Bwana Muchanga amesema hayo wakati nchi tajiri zikiwa katika ushindani kuhusu maliasili za Afrika, huku nchi za Magharibi zikitafuta uhusiano mkubwa wa kibiashara na Afrika, na kuwepo kwa ziara nyingi za viongozi wa nchi za magharibi barani zilizofanywa na viongozi wa Ufaransa na Ujerumani, pamoja na makamu wa rais wa Marekani.

Bw Muchanga amekaribisha kutambuliwa kwa matatizo ya Afrika, hasa kutokana na janga la Covid-19, na changamoto nyingine zinazotokana na sababu mbalimbali.

Amesema ni jambo zuri kuwa Kaskazini na Kusini zinataka kutegemeana zaidi, na hali hii inakaribishwa.