Mkutano wa kilele wa G7 wafungwa huko Hiroshima licha ya upinzani mkali
2023-05-22 08:35:12| CRI

Kundi la Nchi Saba (G7) lilifunga mkutano wake wa siku tatu huko Hiroshima nchini Japan jana Jumapili, wakiahidi kuongeza vikwazo dhidi ya Russia kutokana na msukosuko unaoendelea wa Ukraine, licha ya kupingwa na waandamanaji wengi waliokusanyika mitaani.

Kufuatia maandamano yaliyoendelea kwa siku kadhaa, mamia ya waandamanaji kutoka ndani na nje ya Japan waliandamana jana kupinga taarifa iliyotolewa na viongozi wa G7 pamoja na nyaraka nyingine zilizoridhiwa kwenye mkutano huo.

Baadhi ya waandamanaji waliushutumu mkutano huo kuwa wa kivita unaofadhiliwa na umwamba wa Marekani, na kwamba Serikali ya Japan inapuuza maoni ya wahanga wa bomu la atomiki na wakazi wa Hiroshima kwa kuandaa mkutano huo.

Mji wa Hiroshima uliharibiwa vibaya na bomu la atomiki la Marekani wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia.