ITTF: Kurudi tena kwa Michuano ya kimataifa ya mpira wa meza barani Afrika baada ya miaka 84 kuna maana kubwa
2023-05-22 20:39:33| cri

Ofisa mkuu mtendaji wa Shirikisho la kimataifa la mpira wa meza (ITTF) Bw. Steve Dainton amesema Michuano ya kimataifa ya mpira wa meza unafanyika tena barani Afrika, tukio ambalo linaonyesha jitihada za kuufanya mpira wa meza uwe mchezo wa kimataifa.

Fainali ya Michuano ya kimataifa ya mpira wa meza (WTTC) ya ITTF ya 2023 ilifanyika Jumamosi mjini Durban nchini Afrika Kusini, tukio ambalo linamaanisha kuwa michuano hiyo inafanyika kwa mara ya kwanza barani Afrika tangu mwaka 1939.

Bw. Dainton amesema mpira wa meza ni mchezo maarufu kote duniani, ni muhimu kuiletea michuano ya WTTC kwenye kila pembe ya dunia.