Mkutano wa 76 wa Baraza la Afya Duniani wafunguliwa Geneva
2023-05-22 09:01:23| CRI

Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema mkutano wa 76 wa Baraza la Afya Duniani  (WHA) umefunguliwa jana, huku ajenda kuu ikiwa ni kuokoa maisha na kuhimiza afya kwa watu wote.

Mkutano wa mwaka huu utaamua mustakabali wa karibu na muda mrefu wa shirika hilo, ukianzia na bajeti ya programu kwa miaka miwili ijayo, maamuzi muhimu kuhusu ufadhili endelevu na kuboresha michakato na uwajibikaji wa WHO.

Mkutano huo pia utapitia maendeleo, mafanikio na changamoto zilizojitokeza mwaka jana, pamoja na vipaumbele vya siku zijazo katika nguzo kuu za kazi za shirika hilo, ambazo ni huduma ya afya kwa watu wote, matukio ya dharura, kuboresha afya na ustawi.