Bandari za Dar es Salaam, Djibouti na Berbera zimeipiku bandari ya Mombasa katika orodha ya hivi karibuni ya Benki ya Dunia kwenye bandari zenye ufanisi zaidi duniani, ikionyesha hofu ya ushindani ambayo Kenya imekuwa nayo kuhusu Tanzania kuwa njia inayopendwa na wasafirishaji.
Toleo la tatu la Fahirisi ya Utendaji wa Bandari za makontena duniani (CPPI), imeiweka bandari ya Dar es Salaam katika nafasi ya 312 kwa mwaka 2022 kati ya bandari 348 duniani kote zilizofanyiwa tathmini, na bandari ya Mombasa iko katika nafasi ya 326.
Miongoni mwa mambo muhimu ya ripoti hiyo ni Bandari ya Yangshan ya China, imetajwa kuwa katika nafasi ya kwanza katika kipindi hicho, licha ya kuwa ilikumbwa na usumbufu mkubwa uliosababishwa na vimbunga na mambo mengine.