Shughuli ya “China na Afrika ya Kati kushikana mkono kutoa upendo kwa watoto” ilifanyika hivi karibuni katika Ikulu ya Afrika ya Kati.
Shughuli hiyo iliendeshwa na Rais Faustin-Archange Touadera pamoja na Balozi wa China nchini humo Bw. Li Qinfeng, na kuhudhuriwa na watu 200.
Kabla ya maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Watoto, shughuli hiyo imechangia dawa, mabegi ya shule, vifaa vya elimu na michezo kwa watoto yatima zaidi ya 200 kutoka mashirika manne ya kutunza watoto waliohudhuria shughuli hiyo, ili kuwapa upendo na salamu za siku hiyo.