Tanzania kujenga barabara zaidi ili kuchochea uchumi
2023-05-23 08:50:06| CRI

Serikali ya Tanzania jana ilisema itajenga kilomita 2,035 za barabara mpya kote nchini humo ili kuchochea shughuli za kiuchumi.

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi nchini humo Bw. Makame Mbarawa ameliambia bunge katika mji mkuu Dodoma, kuwa ujenzi wa barabara hizo utatumia shilingi za Kitanzania trilioni 3.7, ikiwa ni sawa na dola za Marekani bilioni 1.6, kuanzia mwaka wa fedha wa 2023/2024, na unalenga kufungua mlango kwa nje kwa ajili ya maendeleo ya uchumi wa nchi hiyo.