Xi atoa wito kwa Jumba la Makumbusho la Taifa la Sanaa la China kujenga heshima duniani kote
2023-05-23 14:38:59| CRI

Rais Xi Jinping wa China ametoa wito kwa Jumba la Makumbusho la Taifa la Sanaa la China (NAMOC) kujiendeleza na kuwa jumba la sanaa linaloheshimiwa duniani kote.

 

Rais Xi ametoa wito huo kwenye barua aliyowaandikia wataalam wakongwe na wasanii wa Jumba hilo. Rais Xi pia ametoa pongezi na salamu za dhati kwa wafanyakazi wote wa jumba kuadhimisha miaka 60 tangu kuanzishwa kwake.