Waziri wa mambo ya nje wa China akutana na naibu waziri mkuu wa DRC
2023-05-23 08:15:18| CRI

Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Qin Gang jana Jumatatu amekutana na naibu waziri mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Bw. Christophe Lutundula hapa Beijing.

Bw. Qin amesema China inakaribisha ziara ijayo ya Rais Felix Tshisekedi wa DRC nchini China, na inatarajia kuwa wakuu wa nchi hizo mbili wataweka mpangilio wa ngazi ya juu na kutoa mwelekeo wa kimkakati kwa maendeleo ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili katika kipindi kijacho.

Kwa upande wake Bw. Lutundula ameishukuru China kwa msaada na uungaji mkono wake muhimu kwa maendeleo ya uchumi na jamii nchini DRC katika miaka iliyopita, na kusisitiza kuwa DRC inashikilia kithabiti sera ya kuwepo kwa China Moja.