Tanzania inatarajiwa kuwa mwenyeji wa mkutano wa siku mbili wa Baraza la Madini na Uwekezaji 2023 utakaofanyika Dar es Salaam kuanzia Oktoba 25.
Waziri wa Madini wa nchi hiyo, Doto Biteko amewaambia wanahabari kuwa, Tanzania ni lango la kuelekea fursa kuu ya uwekezaji wa madini katika Afrika Mashariki.
Amesema, baraza la mwaka huu litafuatilia zaidi uwekezaji wa madini wa kimataifa, ikiwemo miradi mipya na uhusiano wa kiwenzi, teknolojia, kanuni na mitaji, na kuongeza kuwa, mazingira mazuri ya uwekezaji pamoja na maliasili nyingi zimeifanya nchi hiyo kuwa kituo cha uwekezaji chenye mvuto.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa baada ya mkutano huo, Tanzania ina maliasili nyingi za madini ambazo ni raslimali muhimu katika kutengeneza magari yanayotumia umeme, miundombinu ya nishati endelevu na teknolojia nyingine safi.