Mkutano Mkuu wa 7 wa ID4Africa umeanza jana mjini Nairobi, Kenya, ambapo nchi za Afrika zinajadili njia za kuharakisha matumizi ya vitambulisho vya kidijitali ili kuboresha utoaji wa huduma za serikali.
Mkutano huo wa siku tatu umekutanisha serikali, wenzi wa maendeleo na wavumbuzi, na unalenga kuwa vitambulisho vya kidijitali ambavyo ni jumuishi, salama na vyenye heshima vinavyotoa kipaumbele kwa mahitaji ya watu.
Akizungumza katika mkutano huo, Katibu wa Kudumu wa Idara ya Uhamiaji na Huduma za Raia nchini Kenya Julius Bitok, amesema Kenya kwa sasa iko katikati ya kuhamisha vitambulisho vya kidijitali kutoka ngazi ya pili hadi ya tatu. Amesema utaratibu wa vitambulisho vya kutegemeka vya kidijitali utaiwezesha serikali kuwa na takwimu sahihi na kupanga uwezeshaji wa huduma sahihi na muhimu za jamii.