Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) kina mpango wa kubadilika na kuwa kituo kikubwa cha Taaluma ya Tiba ifikapo mwaka 2050, baada ya kupokea nyongeza ya dola milioni 45.5 kutoka kwa mradi wa Elimu ya Juu kwa ajili ya Mabadiliko ya Kiuchumi (HEET). Fedha hizo zinatokana na juhudi za serikali pamoja na Benki ya Dunia kuboresha utoaji wa elimu ya juu.
MUHAS ilitaja vipaumbele vyake katika matumizi ya fedha hizo, kuwa ni pamoja na kufufua na kuandaa mitaala, kuelimisha watumishi, kuweka miundombinu ya kisasa ya TEHAMA na mifumo ya kidijitali kwa ajili ya kufundishia na kuboresha kazi za utawala. Pia amesema chuo hicho kinatarajia kuanzisha chuo cha udaktari, kampasi mpya itajengwa Kigoma Ujiji.