UM: Idadi ya vifo vilivyosababishwa na mvua kubwa DRC yafikia 443
2023-05-24 08:57:36| CRI

Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA) jana imesema, idadi rasmi ya vifo kutokana na mvua kubwa iliyosababisha mafuriko na maporomoko ya udongo nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) imeongezeka hadi 443, huku mamia ya watu wakijeruhiwa na wengi hawajulikani walipo.

OCHA pia imesema, mahitaji ya dharura kwa sasa ni makazi na chakula kwa manusura, na ukarabati wa barabara na madaraja pia ni muhimu ili waathirika waweze kufikiwa.