China na Marekani zafanya mazungumzo ya 13 ya viongozi wa vyama vya kisiasa
2023-05-24 08:41:31| CRI

Mazungumzo ya 13 ya Viongozi wa Vyama vya Kisiasa vya China na Marekani yamefanyika jana Jumanne kwa njia ya video, na pande hizo mbili zimefanya mawasiliano ya kina chini ya kaulimbinu ya ushirikiano wa kunufaishana na kuelewana kati ya China na Marekani.

Mkurugenzi wa Idara ya Kimataifa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Bw. Liu Jianchao, alihudhuria na kuhutubia mazungumzo hayo.

Pande hizo mbili zinaamini kuwa, ni muhimu kwa China na Marekani kupatana, na nchi hizo zinapaswa kufanya kazi kwa pamoja ili kurejesha uhusiano kati yao kwenye njia sahihi, ambayo inaendana na matarajio ya pamoja ya watu wa nchi hizo mbili na jumuiya ya kimataifa, na pia itanufaisha vizazi vijavyo.