Rais wa China atuma barua ya pongezi kwa kongamano kuhusu maendeleo ya Tibet
2023-05-24 08:42:13| CRI

Rais Xi Jinping wa China ametuma barua ya pongezi kwenye kongamano kuhusu maendeleo ya Tibet lililofunguliwa jana Jumanne hapa Beijing.

Kwenye barua yake, Rais Xi amesema kuwa furasa za watu ni haki ya msingi ya binadamu, huku maendeleo yakiwa ni nyenzo muhimu ya kuleta maisha bora kwa watu.

Rais Xi amesema anatumai kuwa kwenye safari mpya ya kuijenga China kuwa nchi ya kisasa, Tibet itafuata kikamilifu na kwa makini falsafa mpya ya maendeleo kwenye nyanja zote, kuongeza juhudi za kuhimiza maendeleo yenye ubora wa hali ya juu, na kujitahidi kujenga Tibet mpya ya kijamaa iliyo nzuri na kisasa na yenye ustawi, masikilizano, umoja na ustaarabu, ili watu wa huko waweza kuishi maisha bora na yenye mafanikio zaidi.