Marais wa China na Eritrea watumiana salamu za kupongeza miaka ya 30 tangu kuanzisha kwa uhusiano wa kibalozi
2023-05-24 16:58:00| CRI

Rais Xi Jinping wa China na mwenzake wa Eritrea  Isaias Afwerk leo wametumiana salamu za kupongeza miaka ya 30 tangu nchi hizo mbili zianzishe uhusiano wa kibalozi.

Rais Xi amesema katika miaka 30 iliyopita, uhusiano kati ya China na Eritrea umethibitishwa na mabadiliko ya hali ya kimataifa, na nchi hizo mbili siku zote zimedumisha urafiki wa kidhati, kuendelea kwa pamoja, na kuungana mkono kithabiti katika maslahi zao za kimsingi na masuala muhimu yanayofuatiliwa. Amesisitiza kuwa anatilia maanani sana maendeleo ya uhusiano kati ya China na Eritrea, na kupenda kuhimiza uhusiano huo uwe na kiwango cha juu zaidi siku hadi siku.

Rais Isaias amesema urafiki kati ya Eritrea na China una historia ndefu, na katika miaka 30 iliyopita, uhusiano kati ya nchi hizo mbili umeendelea kupata maendeleo.