Jitihada za pamoja za Tanzania kuandaa AFCON 2027 zalenga kukuza utalii
2023-05-25 21:10:22| cri

Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania amesema ombi la pamoja la Tanzania, Kenya na Uganda kuandaa Mashindano ya 2027 ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) litakuza utalii katika ukanda huo.

Rais Samia amesema AFCON inatazamwa na zaidi ya watu bilioni moja barani Afrika na sehemu nyingine duniani, na michuano hiyo ni jukwaa la kutangaza utalii.