Zambia yafunga mpaka wake na Tanzania na kuathiri wafanyabiashara wa Tanzania
2023-05-25 20:08:58| cri

Watanzania wanaofanya biashara ya mazao ya nafaka na nchi jirani ya Zambia, wamejikuta katika wakati mgumu baada ya Mamlaka nchini Zambia kuzuia shehena za mazao yao na hivyo kuzusha hofu ya kuathiri mitaji yao, kufuatia serikali hiyo kufunga mpaka kama njia ya kujihami na baa la njaa.

Imefahamika kuwa mwaka jana serikali ya Zambia ilinunua shehena ya mahindi kutoka kwa wakulima wake baada ya nchi hiyo kuwa na mahitaji makubwa ya mahindi, hali iliyoilazimu kununua kwa wingi ili kukidhi mahitaji ya wananchi wake katika siku zijazo.

Kufuatia hali ya sintofahamu kuhusu hatma ya biashara zao, mkuu wa mkoa Songwe Dkt Francis Michael amekutana na kuzungumza na wafanyabiashara hao mjini Tunduma, ambapo amewataka kuwa watulivu wakati Serikali inaendelea kufanya mazungumzo na Serikali ya Zambia.