Rais wa China ahutubia ufunguzi wa kikao kikuu cha Baraza la pili la Kiuchumi la Ulaya na Asia
2023-05-25 08:28:31| CRI

Rais Xi Jinping wa China jana Jumatano ameshiriki na kuhutubia kwa njia ya video hafla ya ufunguzi wa kikao kikuu cha Baraza la pili la Kiuchumi la Ulaya na Asia.

Kwenye hotuba yake, Rais Xi amesema dunia ya leo inashuhudia mabadiliko makubwa ambayo hayajawahi kushuhudiwa katika karne moja iliyopita, na mkondo wa kihistoria kuelekea dunia yenye ncha nyingi na utandawazi wa kiuchumi hauzuiliki. Ameongeza kuwa, huu ni mwafaka mpana uliofikiwa na jumuiya ya kimataifa kuhusu kushikilia mfumo wa pande nyingi na kuhimiza maendeleo yaliyoratibiwa kati ya kanda tofauti.

Rais Xi amesema, Ulaya na Asia ni kanda yenye idadi kubwa zaidi ya watu, idadi kubwa zaidi ya nchi na staarabu anuwai kote duniani. Katika dunia ya sasa inayobadilika badilika, namna ya kuendeleza ushirikiano kati ya Asia na Ulaya si kama tu inahusisha maslahi ya watu wa kanda hiyo, bali pia ina athari ya kina kwa maendeleo ya dunia nzima.