Mamlaka nchini Tanzania jana zimesema kuwa zinachukua hatua kusuluhisha mgogoro wa ardhi kati ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania na raia.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Bw. Innocent Bashungwa alipowasilisha makadirio ya bajeti ya wizara yake katika bunge la nchi hiyo amesema, hivi sasa serikali inachunguza ardhi zote zinazomilikiwa na jeshi hilo na kuzitolea hati miliki husika. Ameongeza kuwa, serikali ya Tanzania kwa sasa imemaliza kuainisha theluthi mbili ya ardhi zinazomilikiwa na jeshi.