Marais wa Uganda na Tanzania wamezindua kituo cha kuzalisha umeme kwa nishati ya maji kinachovuka mipaka ya nchi hizo mbili.
Rais Yoweri Museveni wa Uganda na mwenzake wa Tanzania Samia Suluhu Hassan wamezindua kituo hicho chenye uwezo wa kuzalisha umeme cha megawati 16 kinachovuka mpaka cha Kikagati-Murongo katika wilaya ya Isingiro, magharibi mwa Uganda.
Rais Museveni amesema umeme wa bei nafuu unahitajika sana haswa kwa shughuli za uzalishaji, na juhudi za kuondokana na umaskini.
Rais Samia amesema kituo hicho kitatoa umeme wa bei nafuu kwa Tanzania, ili kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kuhimiza ushirikiano wa kikanda.