CMG na Radio na televisheni ya DRC wasaini makubaliano ya ushirikiano
2023-05-26 22:20:57| cri

Mkuu wa Shirika kuu la utangazaji la China CMG Bw. Shen Haixiong, na Mkurugenzi wa Kituo cha Radio na televisheni cha Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC Sylvie, wamesaini kumbukumbu ya maelewano ya Ushirikiano kati ya vyombo vyao vya habari hapa Beijing, huku Rais Xi Jinping wa China na Rais Felix wa DRC wakishuhudia.

Katika miaka ya hivi karibuni pande mbili zimekuwa zikidumisha ushirikiano, na ili kuimarisha zaidi ushirikiano kati ya vyombo vya habari vikuu vya China na DRC na kupanua mabadilishano ya watu kati ya pande hizo, pande zote mbili zimekubaliana kuanzisha utaratibu wa ushirikiano wa mara kwa mara, kuimarisha ushirikiano katika kubadilishana maudhui, utayarishaji-shirikishi wa vipindi, kubadilishana wafanyakazi na uvumbuzi wa kiteknolojia, na kuchangia katika kukuza ushirikiano.