Viongozi wa Umoja wa Afrika (AU) wameonya Afrika haipaswi kuwa "uwanja wa vita wa kijiografia" kwa nchi zenye nguvu duniani, wakati bara hilo likikabiliana na matishio kadhaa ya amani na usalama wake.
Wakizungumza kwenye hafla ya kuadhimisha kumbukumbu ya kuundwa kwa mtangulizi wa AU, Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU) Mei 25, 1963. Mwenyekiti wa kamati ya Umoja wa Afrika Bw. Moussa Faki Mahamat, amesema katika muktadha huu wa kimataifa wa makabiliano ya maslahi tofauti ya kisiasa, nia ya kila upande inatishia kubadilisha Afrika kuwa uwanja wa vita wa kijiografia, na hivyo kuleta hali ya vita baridi.
Bara la Afrika limekuwa jukwaa la vita ya kuwania ushawishi miongoni mwa mataifa makubwa, ambayo yameongeza juhudi zao maradufu tangu mgogoro wa Ukraine uanze miezi 15 iliyopita