Kenya yaadhimisha Siku ya Afrika
2023-05-26 08:56:52| CRI

Kenya jana iliungana na mataifa mengine barani Afrika kuadhimisha Siku ya Afrika.

Sherehe hizo za kuadhimisha miaka 60 tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Nchi Huru za Afrika, ambao sasa unajulikana kama Umoja wa Afrika, zimefanyika huko Nairobi, na kuhudhuriwa na wanadiplomasia kutoka nchi za Afrika nchini Kenya.

Katibu wa Idara ya Biashara nchini Kenya Bw. Alfred Ombudo K'Ombudo amesema kuwa sherehe ya Siku ya Afrika ni tukio muhimu kwa kusherehekea utamaduni wa Kiafrika pamoja na kuimarika kwa bara hilo. Amesema Kenya ina nia ya kukuza biashara ya ndani ya Afrika pamoja na uhusiano wa kibiashara na uwekezaji na mataifa mengine, ikiwemo China, ambayo ni mshirika muhimu wa Kenya.

 Balozi wa Sudan Kusini nchini Kenya Chol Ajonga amesema maadhimisho ya Siku ya Afrika ni ukumbusho wa mapambano ya watu wa Afrika kufikia uhuru wa kisiasa na kiuchumi.