Mvulana wa shule mwenye umri wa miaka 17 wa Nigeria ametangazwa kuweka rasmi wa Rekodi ya Dunia ya Guinness ya kuruka kamba mara nyingi kwa mguu mmoja ndani ya sekunde 30. Philip Solomon kutoka Shule ya Oyemekun katika Jimbo la Ondo, aliweka rekodi hiyo mapema mwaka huu. Alifanikiwa kuruka mara 153, na kupita rekodi ya mwisho iliyowekwa na Rasel Islam wa Bangladesh mwaka 2021 kwa kuruka mara nane zaidi.
Rekodi za Dunia za Guinness zimethibitisha kuwa, wamebadilisha rekodi yake ya kuruka mara nyingi ndani ya sekunde 30 kwa mguu mmoja mapema wiki hii.