China yatoa wito wa kuungana mkono na uratibu wa pamoja wa kimkakati kati yake na Afrika
2023-05-26 08:40:36| CRI

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Bw. Qin Gang amehudhuria hafla ya kuadhimisha Siku ya Afrika jana Alhamisi hapa Beijing, na kutoa wito wa kuimarishwa zaidi kwa ushirikiano kati ya China na Afrika.

Akihutubia katika hafla hiyo, Bw. Qin kwa niaba ya Serikali ya China amepongeza maadhimisho ya miaka 60 ya Umoja wa Nchi Huru za Afrika, ambao sasa inajulikana kama Umoja wa Afrika, akisema kuwa Afrika imekuwa nguvu muhimu yenye ushawishi na hadhi ya kimataifa inayoendelea kupanda.

Bw. Qin amesema, wakati wa kuingia kwenye zama mpya ya kujenga jumuiya iliyo karibu zaidi na yenye hatma ya pamoja kati ya China na Afrika, pande hizo mbili zinahitaji kuimarisha zaidi mshikamano na ushirikiano kuliko zamani.

Ametoa wito kwa China na Afrika kulinda kithabiti haki na maslahi halali ya upande mwingine na kuungana mkono zaidi kwenye masuala yanayohusu mamlaka, maendeleo na heshima ya upande mwingine.