Rais wa china atuma barua ya pongezi kwenye Jukwaa la Zhongguancun
2023-05-26 08:38:55| CRI

Rais Xi Jinping wa China ametuma barua ya pongezi kwa Jukwaa la Zhongguancun la Mwaka 2023 lililofunguliwa jana Alhamisi hapa Beijing.

Kwenye barua yake, Rais Xi amesema wakati raundi mpya ya uvumbuzi wa sayansi na teknolojia na mageuzi ya kiviwanda inapoendelea kupiga hatua, binadamu wanahitaji ushirikiano wa kimataifa, uwazi na kutoa zaidi waliyo nayo ili wanufaike kwa pamoja, kwa ajili ya kukabiliana na changamoto za pamoja za maendeleo.

Rais Xi amesema China iko tayari kushikana mkono na nchi nyingine kwenye kuhimiza uvumbuzi wa sayansi na teknolojia na kuvifanya vihudumie vizuri zaidi watu wa nchi zote.