UM wawaenzi askari wa kulinda amani waliouawa wakati wakitimiza majukumu yao
2023-05-26 10:17:44| CRI

Umoja wa Mataifa umefanya shughuli za kumbukumbu katika makao makuu yake huko New York, ili kutoa heshima kwa askari wa kulinda amani waliouawa wakati wakitekeleza majukumu chini ya bendera ya Umoja huo.

Katibu mkuu wa Umoja huo Bw. Antonio Guterres ameweka shada la maua katika Kumbukumbu ya Walinzi wa Amani ili kuwaheshimu askari wa kulinda amani zaidi ya 4,200 wa Umoja wa Mataifa waliopoteza maisha yao tangu mwaka 1948.

Baada ya hapo, Bw. Guterres aliongoza hafla katika ukumbi wa mkutano mkuu, ambako medali za Dag Hammarskjold zilikabidhiwa kwa wanajeshi, polisi na walinda amani 103 wa kiraia waliouawa wakati wakitekeleza majukumu chini ya bendera ya Umoja wa Mataifa mwaka jana.