FAO yasema Pembe ya Afrika inakabiliwa na ukame na mafuriko
2023-05-28 21:12:42| cri

Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) limesema Pembe ya Afrika hivi sasa inakabiliana na athari za ukame na mafuriko, ambazo zinatishia maisha ya watu.

Mkuu wa tume ya FAO ya Afrika Mashariki Cyril Ferrand, amesema mvua za Machi hadi Mei zilikuwa za kawaida kwa mara ya kwanza baada ya miaka mitatu au majira matano ya ukame, na kusababisha mafuriko yaliyosababisha maelfu ya watu kupoteza makazi yao.

Amebainisha kuwa ukame wa muda mrefu umefanya udongo kukosa uwezo wa kufyonza maji, na hii ni moja ya sababu ya kutokea kwa mafuriko. Amesema nchi zilizoathirika ni pamoja na Ethiopia, Kenya na Somalia.