Jumuiya ya Maendeleo ya Kiserikali ya Afrika Mashariki IGAD imelaani shambulizi dhidi ya walinzi amani wa Uganda wa vikosi vya Tume ya Mpito ya Umoja wa Afrika nchini Somalia (ATMIS), lililotokea Ijumaa iliyopita mjini Bulo Marer katika mkoa wa Lower Shabelle.
IGAD imetoa rambirambi za dhati kwa familia za waliouawa na kusisitiza kuwa inasimama imara na serikali na watu wa Somalia, katika vita dhidi ya ugaidi na juhudi za kujenga Somalia yenye amani na utulivu.
Jumamosi iliyopita jeshi la Uganda lilisema limetuma timu ya wataalamu kuchunguza shambulio la Ijumaa dhidi ya wanajeshi wake nchini Somalia lililofanywa na kundi la wanamgambo wa al-Shabaab.