Umoja wa Afrika (AU) umepitisha Mpango wa utatuzi wa mapambano nchini Sudan ili kusitisha vita nchini humo.
Taarifa iliyotolewa jana na Umoja huo imesema mpango huo ulipitishwa kwenye mkutano wa ngazi ya viongozi wa nchi na serikali wa Baraza la amani na usalama la Umoja wa Afrika uliofanyika Jumamosi. Mpango huo unaeleza mambo sita, ikiwa ni pamoja na kuanzisha mfumo wa uratibu ili kuhakikisha jitihada zote za kikanda na kimataifa zinaratibiwa na kuwa na ushawishi; kusimamisha uhasama mara moja kwa pande zote, shirikishi na wa kudumu, na kuwe na mfumo wenye ufanisi wa kujibu mahitaji ya kibinadamu.
Mkutano huo ulisisitiza umuhimu wa mchakato wa amani wa Sudan chini ya uratibu wa pamoja wa Umoja wa Afrika (AU), Shirika la Maendeleo la Serikali za Nchi za Afrika Mashariki (IGAD), Umoja wa nchi za kiarabu, Umoja wa Mataifa na wenzi wengine.