Ndege ya China C919 yaanza kufanya kazi ya huduma za kibiashara
2023-05-29 08:51:55| CRI

Ndege kubwa ya abiria ya China aina ya C919, iliyotengenezwa na China kwa kujitegemea, jana ilikamilisha safari yake ya kwanza ya kibiashara kutoka Shanghai hadi Beijing, na kuashiria kuingia rasmi katika soko la usafiri wa anga.

Ndege hiyo ya Shirika la Ndege la China Eastern iliruka asubuhi kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Shanghai Hongqiao ikiwa na abiria 128, na kufika kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Beijing mchana.

Hii ni ndege ya kwanza ya China iliyotengenezwa kwa mujibu wa vigezo vya kimataifa, China ikiwa na haki zote za uvumbuzi.

Mkurugenzi wa idara ya masoko na mauzo ya Shirika la Ndege la Kibiashara la China (COMAC) Bwana Zhang Xiaoguang amesema safari hiyo ya kwanza ni sawa na sherehe ya kuja kwa ndege mpya, na ndege hiyo itaendelea kuwa bora kama ikihimili changamoto za soko.