Baraza Kuu la Uchaguzi la Uturuki lamtangaza Erdogan kuwa mshindi
2023-05-29 08:52:40| CRI

Mwenyekiti wa baraza kuu la uchaguzi la Uturuki Ahmet Yener amemtangaza rais wa sasa wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan kuwa mshindi wa duru ya pili ya uchaguzi wa rais.

Bw. Recep Tayyip Erdogan amepata asilimia 52.14 ya kura kwenye duru ya pili ya uchaguzi huku mshindani wake Bw. Kemal Kilicdaroglu wa chama cha mrengo wa kati cha Republican People's Party (CHP) amepata asilimia 47.86 ya kura.

Kwenye duru ya kwanza ya uchaguzi uliofanyika Mei 14, Bwana Erdogan alipata asilimia 49.52 ya kura huku Bwana Kilicdarogu akipata asilimia 44.88. Kutokana na kuwa hakuna aliyepata zaidi ya asilimia 50 ya kura zinazohitajika, duru ya pili ya uchaguzi ilitakiwa kufanyika.

Kwenye uchaguzi wa bunge muungano unaoongozwa na Bwana Erdogan wa People's Alliance, unaoundwa na chama tawala cha Justice and Development Party (AKP) na Nationalist Movement Party (MHP), ulipata wingi wa viti 323 katika bunge lenye viti 600, huku muungano wa vyama sita ukipata viti 212.