Watu watano wamefariki na wengine wengi hawajulikani walipo baada ya boti iliyobeba watu kadhaa kuzama katika Mkoa wa Savannah nchini Ghana.
Mratibu wa Idara ya Kudhibiti majanga katika mkoa huo Bavuk Adams amesema, ajali hiyo imetokea wakati boti iliyokuwa ikielekea Kpandai kugonga shina la mti katika njia yake na kusababisha ufa uliowezesha maji kujaa kwenye boti hiyo na kuzama. Amesema idadi kamili ya watu waliokuwa ndani ya boti hiyo haijajulikana, na kwamba kikosi cha uokoaji kimefanikiwa kuokoa baadhi ya abiria, na juhudi za kuwatafuta manusura wa ajali hiyo zinaendelea.