Kiongozi mpya wa Nigeria Bola Ahmed Tinubu ameapishwa na kuwa rais wa 16 wa Nigeria, katika hafla iliyofanyika mjini Abuja.
Kwenye hotuba yake baada ya kuapishwa, Bw. Tinubu alieleza maono na mipango yake ya maendeleo ya Nigeria, akisisitiza haja ya kuhimiza maendeleo ya uchumi na mapambano dhidi ya ugaidi na uhalifu. Amesema watafanya kazi kuhakikisha kuwa ukuaji wa uchumi unakuwa si chini ya asilimia 6.
Pia alitangaza kukomeshwa kwa ruzuku ya mafuta, ambayo kwa muda mrefu imekuwa mzigo mzito kwa mapato ya serikali, na serikali yake badala yake itaelekeza fedha hizo katika ujenzi wa miundombinu na maeneo mengine ili kuimarisha uchumi.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje Bi. Mao Ning amesema mjumbe maalum wa Rais wa China Bw. Peng Qinghua alihudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais Bola Tinubu.