Jeshi la Sudan na vikosi pinzani vyakubali kurefusha muda wa kusitisha mapigano kwa siku 5
2023-05-30 08:38:45| CRI

Jeshi la Sudan na Vikosi vya Msaada wa Haraka RSF vimekubaliana kurefusha kwa siku tano muda wa makubaliano ya kusitisha mapigano waliyosaini Mei 20 baada ya mazungumzo yaliyofanyika mjini Jeddah, Saudi Arabia.

Pande hizo mbili zimesisitiza dhamira ya kuruhusu raia wote kuondoka kwa usalama kwenye maeneo yenye mgogoro na kulinda vifaa vya kiraia.

Hata hivyo mapigano makali yalizuka mjini Khartoum kati ya pande hizo mbili saa chache kabla ya makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya kufikia muda wake. Kwa mujibu wa mashuhuda, mapigano hayo yalitokea katika maeneo ya kaskazini mwa Khartoum, ambapo jeshi la Sudan lilianzisha mashambulizi ya anga dhidi ya RSF, huku RSF ikijibu kwa makombora ya kutungulia ndege.