China na Afrika zahitaji zaidi kuimarisha mshikamano na ushirikiano kuliko wakati wowote uliopita
2023-05-30 08:36:05| CRI

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bi. Mao Ning amesema kwa sasa dunia inakabiliana na changamoto nyingi, ikiwa nchi kubwa zaidi inayoendelea duniani na likiwa bara lenye nchi nyingi zaidi zinazoendelea, China na Afrika zinahitaji zaidi kuimarisha mshikamano na ushirikiano kuliko wakati wowote uliopita.

Bi. Mao Ning amesema uhusiano kati ya China na nchi za Afrika umefika kwenye kiwango kipya, na kuingia kwenye kipindi kipya cha kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja ya China na Afrika.

Amesema China inapenda kushirikiana na nchi za Afrika, kutekeleza hali halisi yenye pande nyingi, kushikilia kulinda maslahi halali ya kila upande, kuhimiza mambo ya kisasa yenye umaalumu wa kila upande, kuhimiza mageuzi ya mfumo wa usimamizi wa dunia, kujitahidi kutimiza usalama wa pamoja, kuimarisha maingiliano na mawasiliano ya ustaarabu, ili moyo wa ushirikiano wa kirafiki kati ya China na Afrika uenziwe na kuenea nchini China na barani Afrika, kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja ya China na Afrika yenye kiwango cha juu na ya karibu zaidi, na kuweka mfano wa kuigwa kwa kuhimiza jumuiya yenye mustakabali wa pamoja ya binadamu.