Somalia yasema jeshi lake limewaua wapiganaji 8 wa al-Shabaab
2023-05-30 22:18:12| cri

Jeshi la Somalia limewaua wapiganaji wanane wa kundi la al-Shabaab na kukamata wengine wawili katika mkoa wa Galgadud, katikati ya nchi hiyo.

Ofisa wa jeshi hilo Osman Abdullahi amethibitisha tukio hilo, na kusema wapiganaji waliokamatwa ni Mukhtar Mohamed, ambaye ni mkuu wa intelijensia wa kundi hilo katika mkoa wa Galgadud, na Aseyr Mohamed, anayesimamia ukusanyaji wa ushuru.

Kundi la al-Shabaab halijatoa tamko lolote kuhusu tukio hilo ambalo limetokea siku chache baada ya kundi hilo kushambulia kambi ya Tume ya Mpito ya Umoja wa Afrika nchini Somalia katika mji wa Bula Marer, ambako wapiganaji hao wanadai kuwa wameua askari 130 wa Uganda.