China kuendelea kuchangia kutafuta suluhu ya kisiasa ya mgogoro wa Ukraine
2023-05-30 08:43:18| CRI

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bibi Mao Ming amesema pande zote zinazohusika na mgogoro wa Ukraine zimekubali mchango chanya wa China katika kuendeleza mazungumzo ya amani kuhusu mgogoro wa Ukraine, na kuongeza kuwa China itaendelea kutoa mchango wake katika utatuzi wa kisiasa wa mgogoro huo.

Bibi Mao amesema hayo wakati wa mkutano na wanahabari akieleza ziara ya mjumbe maalum wa China katika masuala ya Eurasia za Bw. Li Hui aliyetembelea Ukraine na nchi nyingine.

Kwenye ziara zake nchini Ukraine, Poland, Ufaransa, Ujerumani, makao makuu ya Umoja wa Ulaya na Russia kuanzia Mei 15 hadi 26, Bw. Li alishiriki katika mawasiliano ya kina na kubadilishana maoni na pande zote kuhusu utatuzi wa kisiasa wa mgogoro wa Ukraine.

Msemaji huyo amesema mgogoro wa Ukraine bado uko katika wakati mbaya na China itaendelea kuimarisha mazungumzo ili kujenga maelewano.