Rais Xi ampongeza Erdogan kwa kuchaguliwa tena kuwa rais wa Uturuki
2023-05-30 08:39:02| CRI

Rais Xi Jinping wa China ametoa salamu za pongezi kwa Recep Tayyip Erdogan kwa kuchaguliwa tena kuwa rais wa Uturuki.

Katika salamu zake Rais Xi amesema China na Uturuki, nchi kubwa zinazoendelea na masoko yanayoibukia, zina maslahi mapana ya pamoja. Ameongeza kuwa katika miaka ya hivi karibuni, maendeleo ya uhusiano wa ushirikiano wa kimkakati kati ya China na Uturuki yamedumishwa kwa kasi, na ushirikiano wa kivitendo katika nyanja mbalimbali umepiga hatua chanya.

Rais Xi amesema anathamini maendeleo ya uhusiano kati ya China na Uturuki na yuko tayari kushirikiana na Erdogan ili kukuza maelewano na kusaidiana katika masuala yanayohusu maslahi makuu na masuala yanayofuatiliwa na kila mmoja wao, ili kuhimiza maendeleo endelevu, thabiti na imara ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili.