Waziri wa mambo ya nje wa China afanya mazungumzo na mwenzake wa Zimbabwe
2023-05-30 08:40:20| CRI

Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Qin Gang amefanya mazungumzo na waziri wa mambo ya nje na biashara ya kimataifa wa Zimbabwe Bw. Frederick Shava mjini Beijing, na kutoa wito wa kuendeleza uhusiano kati ya pande mbili.

Bw. Qin amesema China inapenda kushirikiana na Zimbabwe katika kutekeleza makubaliano muhimu yaliyofikiwa na viongozi wa nchi mbili, kusaidiana kuhusu maslahi makuu yanayohusiana na nchi mbili, na kuhimiza kuendeleza uhusiano kati ya pande mbili. Amesema China inaiunga mkono kithabiti Zimbabwe katika kupinga nguvu ya nje kuingilia mambo ya ndani na vikwazo vilivyowekwa dhidi yake, na kuiunga mkono katika kufuata njia ya maendeleo inayoendana na hali halisi ya nchi.

Kwa upande wa Zimbabwe, Bw. Shava amesema Zimbabwe inapenda kuimarisha ushirikiano wa kunufaishana na China kwenye sekta mbalimbali, na kuhimiza kuinua zaidi kiwango cha uhusiano wa kiwenzi wa kimkakati wa pande zote kati ya nchi mbili.