Rais Xi Jinping asisitiza juhudi za kuharakisha kuijenga China kuwa nchi inayoongoza katika elimu
2023-05-30 08:42:32| CRI

Rais Xi Jinping wa China amesisitiza juhudi za kuharakisha kuijenga China kuwa nchi inayoongoza katika elimu.

Akiongoza kikao cha mafunzo cha kikundi cha Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha Kikomunisti cha China, Rais Xi amesema lengo hilo ni utangulizi wa kimkakati wa kujenga nchi kubwa ya kisasa ya ujamaa katika pande zote, na ni uungaji mkono muhimu wa kufikia hali ya kujiamini zaidi na kuwa na nguvu kwenye sayansi na teknolojia, na ni njia bora ya kuhimiza ustawi wa pamoja kwa wote.

Rais Xi alitoa wito wa kuharakisha uboreshaji wa sekta ya elimu ili kutoa uungwaji mkono mkubwa kwa ajili ya kuendeleza ufufuaji wa taifa la China katika nyanja zote.

China ina mfumo mkubwa zaidi wa elimu duniani, na imejiunga na nchi zenye kiwango cha juu kati katika suala la kiwango cha jumla cha elimu ya kisasa.

Rais Xi amesema China inashika nafasi ya 23 katika faharisi ya elimu duniani, ikiwa imepanda kwa nafasi 26 kutoka mwaka 2012.