China kuzisaidia nchi zinazoendelea kwa kupeleka timu za wafanyakazi wa afya
2023-05-30 19:17:45| cri

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Mao Ning amesema, China itaendelea kuzisaidia nchi zinazoendelea na kuboresha afya na maisha ya watu duniani kupitia timu za wafanyakazi wa afya wa China ambao kwa sasa wanatekeleza majukumu yao katika sehemu 115 na nchi 56 duniani.

Mao amesema, hivi karibuni, nchi nyingi zimesifu kazi zinazofanywa na wafanyakazi wa afya wa China katika nchi hizo. Amesema miaka 60 iliyopita, China ilituma timu yake ya kwanza ya wafanyakazi wa afya nje ya nchi, na tangu wakati huo, jumla ya wafanyakazi 30,000 wa afya wa China wametibu zaidi ya wagonjwa milioni 290 katika nchi na sehemu 76, zikiwemo nchi za Afrika na Asia, na kupata mafanikio makubwa.