Umoja wa Mataifa wasema Angola ina umuhimu mkubwa kwa utulivu wa kikanda
2023-05-30 20:18:41| cri

Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulika na Operesheni za Ulinzi wa Amani, Jean-Pierre Lacroix, amesisitiza umuhimu wa diplomasia ya Angola katika utulivu wa kikanda.

Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Angola imesema, baada ya mkutano na Waziri wa Wizara hiyo, Tete Antonio mjini Luanda, Lacroix amesema Angola ina nafasi muhimu katika kuchangia zaidi operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa. Pia amesisitiza ushirikiano wa kina kati ya Angola na Umoja wa Mataifa, hususan katika operesheni za ulinzi wa amani.