Changamoto ya umeme nchini Tanzania kuwa historia
2023-05-31 20:26:08| cri

Waziri wa Nishati nchini Tanzania, Januari Makamba, amesema Serikali ya nchi hiyo ipo katika mikakati kwa kipindi cha ndani ya miaka miwili kuhakikisha kuwa tatizo la upatikanaji wa umeme nchini humo linakuwa historia.

Makamba ameyasema hayo kwenye maonyesho ya Wiki ya Nishati yanayoendelea nchini humo, na kuongeza kuwa ni kweli suala la umeme bado halijatengemaa lakini kupitia mpango huo litamalizika.

Kuhusu uzalishaji wa umeme nchini humo, Waziri Makamba amesema umeongezeka kwa asilimia 11 kwa mwaka, ikilinganishwa na mwaka jana ambako kulikuwa ongezeko la asilimia 5.